Wakati kuna tamaa, hakuna kisichowezekana

Unataka kujua hadithi yangu? Nifuate kwa karibu.

Mimi ni Madeleine Kasiba, msichana niliyezaliwa katika familia ya watoto kadhaa ambapo mimi ni wa 3 katika familia hiyo. Nilizaliwa nikiwa na udhaifu kwenye kiuno, ambao ulinipa ulemavu huu ambao ninaniumiza ùoyoni lakini nime kubali jinsi nilivyo.

Hansen avec Madelaine le jour de lan distribution de kit scolaire

Kwa bahati mbaya katika familia, ikiwa wewe ni mlemavu, wanafamilia huwa wanakuacha kwa sababu wewe ni mzito kidogo kwa sababu ya kukosa kutembea mwenyewe. Kwa hili, kuna unyanyapaa wa mtu mwenye ulemavu, ubaguzi katika masomo na wakati mwingine kuachwa kabisa.

Katika kesi yangu, familia inanijali, lakini sio kama watoto wengine wa kawaida. Huwa nakaa nyumbani kuchunga nyumba na watoto ambao wamenifuata. Baadhi ya wanafamilia hawakutaka niende shule. Lakini nilitaka kwenda shule kama watoto wengine wa kimo changu na Mama yangu alisisitiza kila mara nisome. Hivi ndivyo nilivyoandikishwa katika shule ya karibu yetu, pale EP MASANGANO, na mkuu wa shule alinipenda sana. Pamoja na suala la malipo ambayo wazazi wetu wanalipia katika masomo ya watoto wao, wakati fulani kulikuwa na ugumu wa kutulipa karo na walitaka kuniacha nyumbani kwa kuhofia kushindwa kunilipia masomo. Katika kiwango cha darasa la 4 kulitokea Bwana Hansen Kaseke ambaye ni meneja wa Tree for Hope and Life, ambaye alikuwa ametulipia vifaa vya shule na karo kwa watoto 25 ambao walikuwa hawana matumaini ya kuendelea. Nilipoanza kusoma bila kufukuzwa shule, nilifufua azma ya kusoma katika ngazi ya shule ya upili. Nilimaliza shule ya msingi bila kulipa hata senti. Leo nipo Sekondari darasa la 7. Ninaamini nitaendelea kwa kiwango cha fursa na msaada ninaopokea. Siku moja nitakuwa mkunga au mwanasayansi wa kompyuta ili kuwasaidia wengine kama mimi kuwa muhimu katika jamii. Shukrani zangu kwa marafiki na wafadhili wa ndani na wale kutoka Ujerumani wanaoturuhusu kusoma na kutimiza ndoto zetu za utotoni.

Mady Kasiba